Licha ya watu kumchukia Chriss Brown kwa tabia zake sasa kibao hicho kimeamia kwa msanii justine Bieber ambae ameandamwa sana na majirani zake baada ya majirani hao kupiga kelele za kuomba msaada kupitia vyombo vya habari wakimtuhumu mwimbaji huyo kugeuka kero na kuvuruga utulivu ktk maeneo hayo kwa tabia yake ya kuendesha gari kwa kasi, kupiga kelele na kuvuta marijuana mbele ya watoto, kilio chao kimefika mbali baada ya gari la msanii huyo kuingia mikononi mwa polisi.
Lakini ripoti kutoka chanzo cha kuaminika upande wa polisi ni kwamba baada ya mahojiano ya muda polisi hao walimpa onyo kijana huyo na kumruhusu aendelee na safari yake.
Hivi karibuni majirani zake Justin Bieber walilalamika na kutishia kumfungulia mashtaka kwa kuwa huwapigia kelele nyingi akiwa anarudi kutoka club na rafiki zake, lakini pia huendesha gari lake kwa kasi sana wakati yuko katika eneo la makazi ya watu, na tuhuma mbaya zaidi ni kwamba huvuta marijuana mbele ya watoto wao wenye umri mdogo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni