Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies.com mwanadada Jacqueline wolper alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au michango mbalimbali kupitia account hizo feki
“Leo nilikuwa naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja na hela? Nikawa sijui cha kumwambia maana sikumuagiza viatu na wala sijampigia simu kumwambia anitumie hela, ndipo aliponionesha huo ujumbe kwenye simu yake na ndio nikagundua hizo account feki za hao watu wanaoutumia jina langu kutapeli watu” Alisema Jack.
“Mimi sipo facebook na wala sitarajii kujiunga, nawaomba sana mashabiki wangu wajue hilo. Natumia mtandao wa instagram kwa jina la wolpergambe au jacklinewolperjacklinewolper.” Alisisitza Wolper
Pia alisema kuwa amendundua leo kuna mtu mwingine anayetumia jina lake kuomba watu wamchangie kuhusu kampeni inayoitwa “Zinduka” na amewataka sana mashabiki wake wasije wakafanya hivyo kwani mtu huyo ni mwizi na analengo la kumchafulia jina lake.
(Picha za account account feki za hao matapeli)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni