Jumatatu, 3 Juni 2013

MIMBA YA DIAMOND YAMTESA PENNY, AZIDIWA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI....




TUMEINYAKA kwamba mimba anayotamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa amempachika mpenzi wake, Peniel Mungilwa ‘Penny’, inadaiwa kuanza kumtesa mtangazaji huyo wa DTV.

Penny akiwa hospitali. Habari zisizokuwa na chenga kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa mrembo huyo, zilieleza kwamba kufuatia hali hiyo, Penny alikimbizwa kwenye Hospitali ya Regency, Dar wikiendi iliyopita kisha akalazwa, akachomwa sindano na kutundikiwa dripu.

 

Diamond na Penny katika pozi. Akizungumzia hali hiyo, Penny alisema kuwa ni kweli alizidiwa usiku na alikimbizwa hospitali ambapo pamoja na mengine lakini kubwa vipimo vilionesha kuwa alikuwa na malaria.

Hata hivyo, habari tulizozipata wakati tunakwenda mitamboni zilieleza kuwa Penny aliruhusiwa kutoka hospitalini na anaendelea vizuri.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni