Jumatano, 12 Juni 2013

HUU NDIO MJENGO WA GHOROFA MOJA ANAOMILIKI MASANJA HUKO TABATA

Ama kwa hakika kama tutakuwa na akili za kukumbuka kuwekeza basi hatakuja kutokea msanii akalalamika amekufa maskini .tunajua kuwa bada sanaa yetu ipo chini haithaminiwi lakini basi ni vyema wasanii kujua kuwa hakuana msaada wowote zaidi ya nguvu juhudi na akili zako.
Kwa upande mwingine tuseme wasanii tumejisahau sana na kuitupia serekali mzigo japo sikatai kuwa hawauhusiki wanahusika tena kwa asilimia kubwa lakini tunapoona hawasikii hawajali unadhani nini cha kufanya je tukae tu kupiga kelele huku siku zinakwenda na kuambiwa wasanii wanakufa maskini?Hapana mi nadhani tufuate mifano ya wenzetu kama masanja,Diamond,Ray,Lade jayde,Prof.jay ,Dotnata,Rich Rich na wengine wengi ambao pamoja na serekali kujifanya haisikii kilio cha wasanii ila wao wameamua kujiwekeza na kwa hakika wamefanikiwa.
Huu ndio mjengo wa ghorofa anaomiliki masanja mkandamizaji huko tabata

Akizungumza na thesuperstarstz kwa nja ya simu moja ya watu wa karibu na masanja amesema kwasasa masanja anamiliki kampuni kubwa ya ulinzi yenye zana madubuti na silaha za kisasa katika ulinzi pia ana mmbwa wakutosha na ana walinzi kibao aliowajiri kwasasa hii inatupa picha kuwa sanaa kama tutatumia akili basi inarudisha fadhila kwako.

Kusema kweli thesuperstarstz inakupongeza sana masanja kwa hatua uliyofikia na pia tunakuombea mungu akupe zaidi na zaidi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni