Jumamosi, 27 Julai 2013

DUDE ANASWA LAIVU AKIWA NA KIMWANA MWINGINE

STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amenaswa na demu mwingine aitwaye Mboni Mhando tofauti na mkewe anayeshi naye, Eva. Dude na demu huyo aliyebainika kuwa ni msanii, walinaswa juzikati katika Hoteli ya Traventine Magomeni, jijini Dar wakijivinjari katika mikao ya kimalovee ambapo paparazi wetu alitumia kifaa maalum cha kupigia picha na kuwanasa bila wao kujijua.

Baada ya kuzinasa picha hizo, mpiga picha wetu alimvaa Dude na kumuuliza kulikoni agandane na demu huyo wakati ana mkewe nyumbani, alichomoa kuwa siyo demu wake bali ni msanii mwenzake eti wanapanga mipango ya kazi.

Hapa tulikuwa tunapanga mipango ya kufanya filamu, huyu ni msanii tena wa siku nyingi sababu aliwahi kucheza kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu miaka ile,” alisema Dude huku akimsihi mpiga picha afute picha kama amekwisha piga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni