Jumamosi, 27 Julai 2013

STARS WAKIWA MAZOEZI KUPAMBANA NA CRANE LEO


Wachezaji mbalimbali wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Satrs' ambao wanasakata kabumbu ndani ya nchi wakijifua katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo Nambole nchini Uganda. Stars ipo nchini Uganda na kesho inataraji kushuka katika dimba la uwanja huo kumenyana vikalina The Crenes ya Uganda kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani CHAN.

Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni