Ijumaa, 31 Mei 2013

Big Brother: mume wa boss lady Zari wa Uganda kutoangalia Big Brother, kisa ex wa mkewe ni mshiriki

Msimu wa 8 wa Big Brother Africa ‘The Chase’ unazidi kushika kasi, sio tu kwa washiriki lakini hata kufichua nyeti za chini ya kapeti ambazo kama si Big Brother leo hii huenda nisingekuwa naandika habari hii.
Mume wa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa nchini Uganda Zari aitwaye Ivan Ssemwanga, mara baada ya show ya ufunguzi wa shindano la Big Brother Jumapili (May 26) kuanza, alisema hataangalia Big Brother baada ya kugundua kuwa mpenzi wa zamani wa mkewe Zari , staa wa basketball aitwaye Isaac Lugudde LK4 ambaye ni mwakilishi wa Uganda yuko mjengoni, hivyo ni kama tusi kwake.

Wakati akitazama ufunguzi huo kabla washiriki hawajafahamika, Ivan alimuona mshiriki wa kwanza kupanda kwenye stage, bibie Pokello wa Zimbabwe, ambaye alimchagua mpinzani wa Ivan aitwaye Isaac kama mwanaume wa kuingia naye. Baada ya kitendo hicho Ivan aliamua kuswitch kwenye movie na kutweet “Chillin in ma cinema room watching Temptations by Tyler Perry” akiashiria haangalii tena BBA.

Uhusiano wa Zari na Isaac ulikuja miezi kadhaa iliyopita baada ya Zari na mumewe kuachana kwa muda na baadae walikuja kurudiana.

Siku moja baada ya reality show hiyo inayoendelea huko Afrika Kusini kuanza rasmi, msichana mrembo na tajiri wa nchini Uganda ‘boss lady’ Zari Hussein alionyesha jeuri ya pesa kwa kusema hawezi kushindania $300,000 za Big Brother ambazo hazifikii hata thamani ya moja ya magari anayotumia ambayo ni $ 389,500!! Hey peeps! Huyu manzi anamiliki Lamborghini among others.

source: bongo5

Justin Bieber matatani, gari lake sasa lashikiliwa na polisi kisa hiki hapa

Licha ya watu kumchukia Chriss Brown kwa tabia zake sasa kibao hicho kimeamia kwa msanii justine Bieber ambae ameandamwa sana na majirani zake baada ya majirani hao kupiga kelele za kuomba msaada kupitia vyombo vya habari wakimtuhumu mwimbaji huyo kugeuka kero na kuvuruga utulivu ktk maeneo hayo kwa tabia yake ya kuendesha gari kwa kasi, kupiga kelele na kuvuta marijuana mbele ya watoto, kilio chao kimefika mbali baada ya gari la msanii huyo kuingia mikononi mwa polisi.


Ripoti zinasema gari la mwimbaji huyo aina ya Farrari lilisimamishwa na polisi nje kidogo ya geti la Bieber sababu ikiwa ni mwendo kasi uliopitiliza kwa kuzingatia kuwa yuko katika maeneo ya makazi ya watu. Lakini bahati nzuri Bieber mwenyewe hakuwa na gari hilo siku hiyo na lilikuwa linaendeshwa na rafiki yake aliyefahamika kwa jina la ‘Lil Twist’.

Lakini ripoti kutoka chanzo cha kuaminika upande wa polisi ni kwamba baada ya mahojiano ya muda polisi hao walimpa onyo kijana huyo na kumruhusu aendelee na safari yake.

 Hivi karibuni majirani zake Justin Bieber walilalamika na kutishia kumfungulia mashtaka kwa kuwa huwapigia kelele nyingi akiwa anarudi kutoka club na rafiki zake, lakini pia huendesha gari lake kwa kasi sana wakati yuko katika eneo la makazi ya watu, na tuhuma mbaya zaidi ni kwamba huvuta marijuana mbele ya watoto wao wenye umri mdogo.

Cheki hapa Picha alizopiga mrembo Cassie's kwajili ya Esquire Magazine





MABADILIKO KUHUSU MAZISHI YA NGWEA


Habari kutoka kwa wanakamati wa mipango ya mazishi ya marehem Albert Mangwea zinasema kuwa mwili wa marehem Ngwea utafika Dar siku ya jumapili saa nane mchana na sio jumamosi kama ilivyoarifiwa hapo awali…

Mwili huo utaagwa siku ya jumatatu saa mbili mpaka saa sita machana ambapo safari itaanza kuelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi

MZUMBE SECONDARY YAFUNGWA...WANAFUNZI WAPEWA SIKU MBILI WAPOTEE KATIKA MAZINGIRA YA SHULE

Wananfunzi wakidato cha kwanza hadi cha sita katika shule ya sekondari Mzumbe Morogoro wamelazimika kuandamana kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa huo wakishinikiza kuboreshewa huduma muhimu.

Maboresha wanayodai kuboreshewa shuleni hapo ni pamoja na miundombinu, kuondoa ubadhirifu, uongozi mbovu na kukomeshwa vitendo vya lugha chafu zinazo tolewa na baadhi ya walimu.

Maandamano hayo yalizimwa mapema asubuhi baada ya jeshi la polisi kulazimika kufika katika eneo la
sangasanga barabara kuu ya Iringa Morogoro ambapo maandamano hayo yalikuwa yamefika kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro.

Wananfunzi hawa wa shule ya sekondari Mzumbe Morogoro ya wenye vipaji maalum wanadai kuwa maandamano hayo yanatokea baada ya kuvumilia kwa muda mrefu na hivyo wameamua kupaza sauti zao wakibainisha matatizo lukuki yanayo wasibu ambayo yanaweza kushusha kiwango cha taaluma yao.

Mkuu wa shule ya sekondari Mzumbe Dismas Njawa ameelezea namna alivyoweza kutatua baadhi ya matatizo lakini hayakukidhi haja za wanafunzi hao.

Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Elia Ntandu alilazimika kwenda kuzungumza na wanafunzi hao akiahidi kuyafanyia kazi yale yatakayo wezekana.


Wanafunzi hawakuelewa, na ndipo Serikali ilipoamua kuifunga shule ya Sekondari ya vipaji maalumu, Mzumbe kwa muda usiofahamika na kuwapa wanafunzi siku mbili, kuanzia leo, kuondoka shuleni hapo
---
Monica Lyampawe,
TBC Morogoro.

ZANZIBAR YAPIGA MARUFUKU NDOA ZA JINSIA MOJA.....UKINASWA IMEKULA KWAKO ( MIAKA 30 JELA )

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu.

Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.

Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.

MWAKILISHI WA TANZANIA BBA ALIVYOJIACHIA NA MSHIRIKI TOKA NAMIBIA


Kwa upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah
Monroe alipata nafasi ya kushare na Denzel mawili
matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa
ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. Jana
Huddah alifunguka na kumwambia kuwa anahitaji
mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a
gold digger. Lakini second kadhaa baadae
akafuta kauli yake na kumwambia kuwa
alikuwa anatania. Really?!

Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na
Natasha wako katika nafasi kumbwa na Eviction.


KIJANA ANUSURIKA KUFA BAADA YA VIBAKA KUMCHOMA MOTO HUKO MKOANI LINDI

 Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Ismai Mayoba(31) anayefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Manispaa ya Lindi amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto.
Kwa sasa kijana huyo amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.

 Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.

Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndugu Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie Moto huku akijua ni kosa kisheria.

Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAYA HAPA

                                Matokeo ya kidato cha sita ...Ukitaka kuyaangalia bofya                                                 BOFYA HAPA

HII NDIO VIDEO INAYO ONYESHA UCHAFU UNAO ENDELEA BIG BROTHER AFRICA

trong>Hii ni video inayoonesha uchafu unaotendeka ndani ya jumba la Big Brother Africa....
                                                                                                                                                                        JIONEE MWENYEWE HAPA   
             

FAMILIA YA ALBERT MANGWEA YATOA TAARIFA KUHUSU MABADILIKO YA RATIBA YA MAZISHI

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa
msemaji wa Familia,ambae ni
Kenneth Mangwair,Kuwa mwili autowasili tena
Tarehe 1 mwezi wa sita alasiri
kutoka nchini South Afrca......
kama ilivyotegemewa bali,utawasili siku ya Jumapili
tarehe 2 ya mwezi wa Sita
2013 alasiri.......
Hii imetokana na Watanzania waishio Nchini South
Africa kuomba kwa Familia
nao kupewa nafasi kutoa Heshima za mwisho kwa Super
Star huyo wa Muziki wa
Bongo......kwa mara ya mwisho katika safari ya mwisho
ya Ndugu yetu Albert Mangwair....

Endelea kutembelea this is diamond kupata official
updates zote za msiba
huu kwenye tasnia ya muziki wa Bongo,Albert Mangwair.....!!

Mshiriki wa Big Brother Africa Kutoka Zimbabwe Aingia Kwenye Kashfa Baada ya Kusambaa kwa Picha Zake za Ngono


One of the housemates representing Zimbabwe in the ongoing BBA – The Chase, Pokello Nare has been hit by a sèx tape scandal a few days after she entered the BBA house.

According to Peacefmonline.com investigations, the said sex tape was acted and recorded by Pokello and her boyfriend Desmond Chideme also known as Stunner who is popular urban grooves artiste.

Stunner is famous for his role in a leaked sex tape in which he had sex with his socialite girlfriend Pokello Nare. In the video, he is seen having sex without protection with the girl that he is not married to. The ‘Godo’ hit maker also went public as he got circumcised in a bid to promote education on HIV/AIDS and how to prevent the Aids scourge.




Asked what viewers can expect from her, she says: “I am beautiful, intelligent, controlling and entertaining. I am funny and witty and I say the most humorous things.

Pokello says if she wins the USD 300 000, she’ll buy a big house for her son and herself, send him to a full-time soccer academy in London and invest in her business.

RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEA KUTOKA KWA KAKA WA MAREHEMU

Baada ya kumalizika kwa uchunguzi, uliokuwa ukifanyika
katika hospitali ya Hillbrow, mwili wa marehemu Albert
Mangwea(Pichani) unatarajiwa kuwasili Jumamosi kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya kusini,
ukitokea nchini Afrika ya kusini.
Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali
ya muhimbili kuhifadhiwa, uletwaji wa mwili huo, ni
kwa hisani ya Clouds
Media Group. Ndio waliogharimia safari ya
mwili wa marehemu.

Jumapili asubuhi, kuanzia saa mbili, mwili wa Albert
Mangwea utakuwa unaagwa viwanja vya leaders
club na kampuni
itakayoshughulikia
zoezi hili ni Entertainment Masters na baada
ya mwili kuagwa,
safari ya kumsindikiza Albert Mangwea
kuelekea kwenye maziko
itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro.

Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la
Kihonda, mkoani,
Morogoro...!!

Alhamisi, 30 Mei 2013

P Funk Majani Leo Aamua Kupasua Jipu Kwa Ukweli Uliomfanya Apige Stop Clouds Fm


MAHOJIANO KATI YA Dan Chibo (DC) wa TBC FM na P funk majani.
Leo nilipata fursa ya kuongea na mmoja kati ya maproducer wakongwe kwenye tasnia ya Muziki wa hapa Bongo aitwaye P Funk Majani.
Mahojiano yalikuja mara baada ya taarifa zilizosambazwa mapema leo kwamba Producer huyo amekataza nyimbo zilizorekodiwa na Mwanamuziki aliyefariki nchini Afrika Kusini jana Albert Mangwea kuwa zisipigwe kwenye kituo cha Clouds Fm.

Mbali na mambo mengine nilitaka kujua ukweli na undani juu ya taarifa hiyo na haya ndio yalikuwa maongezi yangu na P Funk Majani...



DC: Je ni kweli kwamba umekataza Nyimbo za Ngwear zilizorekodiwa Bongo Record kuwa zisipigwe Clouds Fm..?

P Funk Majani: Hiyo ni kweli kabisa, mimi nimekereka na hili jambo kwanza kwa sababu mimi na Mangwea tumejuana miaka kibao na tumeongea mengi, so mimi nnachojua uamuzi niliochukua ni kitu ambacho yeye mwenyewe angependa na angetaka iwe hivyo....


Kwa sababu kila siku alipokuwa anakuja studio malalamiko yake ilikuwa ni kuhusu hawa hawa watu kila siku....

Umenielewa..? so ni hicho kilichokuwa kinatajika kufanyika, na mi mwenyewe sifurahi wao wafaidike, sasa hivi ambaye amefariki mtu wetu ambaye tunampenda nyie mnachukulia biashara wanatangaza, wanafanya nini, wanapiga na nyimbo, alipokuwa hai mbona mlikuwa hamumsaidii....



Mlipokuwa mnajua labda ana matatizo ya kutumia madawa ya kulevya mbona hamjamsaidia kumsaidia kumchangia kama Ray C sijui nani kumpeleka nje au wapi asafishwe basi......

So…! Vitu kama mimi basically nimechoka utawala wao sababua wao mchezo wao ni kuchezea wasanii vichwa kuwapa stress na kuwaangamiza kimaisha.....

Umenielewa… kwa udulumati wao, udhulumati wao umezidi so ndio hicho kinachosababisha watu wahanganyikie kimaisha, umenielewa…?


Kukosa fedha na kuweza kutimiza mahitaji ya maisha lazima uchanganyikiwe, unakimbilia vitu vitu suala za pombe au sijui madawa ya kulevya au nini inategemea na mtu moyo wako una nguvu kiasi gani cha kudhibiti hivi vitu.



DC: Unataka kusema kwamba jamaa ndio wamesababisha kifo chake…?


P Funk Majani: Siwezi kusema asilimia 100 wamesababisha lakini mchango mkubwa wa frustration, frustration, unajua kitu frustration…? Siwezi ku-accuse, si-accuse lakini hiyo ni maoni yangu mimi, kutokana na yale maongezi niliyokuwa nae nikikaa na mdogo wangu Mangwea, umenielewa….?

Najua kabisa alichokuwa ananiambia na vitu ndio vimemsababisha aingie huko, sasa mimi ndio sitaki kwa ufupi, kama nimekosea mtanisamehe bwana….

DC: Je umewataarifu rasmi..?

Nimeanza kwa kupiga simu kwa sababu ni asubuhi nimeamka vile nimewafahamisha, nimewaambia vizuri, nilivyowaletea hizi nyimbo niliwaletea bila mkataba au karatasi yoyote mmezipiga....


So... kwa sasa hivi kwa ustaarabu naomba nnavyowaomba acheni msizipige, na mi ntaleta official barua, nimeshaongea na Cosota, eeh watai-stamp Wakili ndio ataiandika barua inapelekwa vizuri na vitu vinaendelea, kama wao ni wastaarabu itabidi waelewe.

UPDATE; HISTORIA YA MSANII ALBERT MANGWEA KWA UFUPI

Albert Mangwea ni Mngoni kutoka Songea, alizaliwa Mbeya Novemba 16 1982 kisha 1987 wazazi wakahamia Morogoro ambako familia iko mpaka leo.

Alianza kuandika verse yake ya kwanza mwaka 1996, album yao ya kwanza waliipeleka kwa MAMU mwaka 1998 yeye na Mez B wakiwa form two.

 Ngwea aliingia studio mara ya kwanza Marimba Studio, album yao ya kwanza na Mez B inaitwa 'Heshima kwa wote' wakimshirikisha Dudubaya

Unaweza kushea post hii na wengine wapate taarifa mtu wangu, Usimamizi wa utoaji wa taarifa hizi unafanywa na fastjet Vodacom Tanzania na CRDB Bank Plc


MITINDO:FLAVIANA MATATA ALAMBA DILI NONO TRUWORTHS


Miss Universe 2007,Flaviana Matata week moja imepita tangu alambe donge nono
la kuwa Model ndani ya Kampuni ya kutengeneza mavazi ya aina mbalimbali
TRUWORTHS na Juzi kati aliweza kupiga picha za kwanza kama model wa
TRUWORTHS baada ya kusaini mkataba huo Nchini South Africa...
Flaviana aliezaliwa Mwaka 1988,June 9 shinyanga nchini Tanzania...
Alishinda Miss Universe Tanzania na alienda kukupeperusha bendera
ya Tanzania na kuwa Mshindi wa 6......Flaviana matata ameshiriki mashindano
mengi ya urembo ikiweno Runway ya kwanza chini ya Mwanamitindo
Mustapha Hassanali,Vivienne Eastwood,Tory Burch,Suno & Louise Gray na
Mshirika wake wa Nguvu Alexander McQueen......

This Is Diamond inamtakia Mafanikio na Baraka tele kwenye
kazi yake ya Unamitindo
afike mbali kuipeperusha Bendera ya Taifa Letu Tanzania....




“Sikuwahi kumsaliti Diamond na tulikuwa tunapendana sana”

Miss Tanzania mwaka 2006 na muigizaji wa filamu Wema Sepetu amefunguka kupitia jarida jipya la Mzuka kuwa katika uhusiano wake wote na Diamond hakuwahi kumsaliti.
Wema ambaye yupo kwenye cover la jarida hilo linalotolewa na kampuni ya Bongo5 Media Group, amefunguka kwa kusema kuwa yeye na Diamond walikuwa wakipendana sana. “Maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo,” amefunguka Wema. Wema amefunguka pia kuhusu jinsi Diamond alivyomcheat na Jokate kwa kusema, “nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza.” Katika jarida hilo ambalo linauzwa kwa shilingi 1,500 tu, Wema amesimulia mengi tangia alipokutana na Diamond, jinsi alivyoumizwa na kitendo chake cha kumrekodi na kusambaza sauti kwenye radio, mapenzi yake na Kanumba, utajiri wake, jinsi anavyowapenda mbwa wake na mambo mengine exclusive. Usikose Kusoma Jarida Hilo La Mzuka kwa sh.1500 tu

source:.bongo5 (246)

DOWNLOAD JORABA - HAWATAKI


ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (4)

Click hapa kuangalia matokeo ya kidato cha nne (4) BONYEZA HAPA

Jumatano, 29 Mei 2013

Sikiliza/download wimbo mpya wa maombolezo – “R.I.P Brother Ngwair”

Nyimbo maalum, by Mozeh Thomas & Mirror Rhymes, ya kuomboleza kifo cha msanii wa Bongo flava, Albert Mangwea aka Ngwair, aliyefariki jana nchini Afrika kusini.

Song: R.I.P Brother Ngwair
Artists: Mozeh Thomas & Mirror Rhymes
Studio: Overclassic Music
Producer: Eizer
Unaweza kusikiliza au download hapa chini
<iframe id="hulkshare-player-embed" name="hulkshare-player-embed" src="http://www.hulkshare.com/hsPlayer/embed/embed_clean.php?fn=y33r3ck1mdc0&enableDownload=1&enableAdd=false&bg=000000&fg=undefined&iconColor=8CDA27&backColor=000000&outColor=CCCCCC&overColor=FFFFFF&textColor=9E9D9D&tintColor=373737&type=7&width=100%" scrolling="no" frameborder="0" allowTransparency="true" style="width:100%;height:197px;"></iframe><iframe id="hulkshare-player-embed" name="hulkshare-player-embed" src="http://www.hulkshare.com/hsPlayer/embed/embed_clean.php?fn=y33r3ck1mdc0&enableDownload=1&enableAdd=false&bg=000000&fg=undefined&iconColor=8CDA27&backColor=000000&outColor=CCCCCC&overColor=FFFFFF&textColor=9E9D9D&tintColor=373737&type=7&width=100%" scrolling="no" frameborder="0" allowTransparency="true" style="width:100%;height:197px;"></iframe>

Taarifa Juu ya Mazishi ya Albert Mangwea Morogoro na Jinsi Mwili Utakavyofika Hapa Tanzania

Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach. Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa. Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa. Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifau 


Salamu za wasanii na wa bongo movies kufuatia kifo cha mwanamuziki Albert Mangwea

Zifuatazo ni baadhi ya salamu na maneno mbalimbali yaliyosemwa na baadhi ya wasanii wa bongo movies kupitia mitandao tofauti ya kijamii baada ya kifo cha mwanamziki wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea kilichotokea huko Afrika ya kusini leo.
Jokate Mwagelo alikuwa mtu wa kwanza kwanza kutweet kwa kuandika…
Sad news ...... Mkali wa freestyle #RIPNgwea
Jaquiline wolper kupitia instagram naye ameandika
“mangwea mungu ailaze roho yako mahali pema peponi”
Elizabeth Michael (LULU) naye ameandika…..
“Kuna kipindi inatupasa kuamini na kuelewa kuwa sisi sote ni mali ya Mungu....tumeubwa ili tuishi na mwisho wa maisha kuna kifo!!Naamini wengi wetu inakuwa ni vigumu kuamini lakini inatupasa kuamini na kumshukuru Mungu pia!!Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la bwana lihimidiwe....!!!Rest In Peace "Mangwair"safari yetu ni moja mbele yako nyuma yetu!!!AMEEEEEN”
Salma Jabu (Nisha) naye ameandika
“I cant explain how i feel ,,R.I.P brother mangweir daah!!!!!!!!! Xo sad”
Wema Sepetu akaandika….
“Oh God! Rest Alz soul in eternal peace,we loved him but u love him more.kazi ya mola daima haina makosa”
Mipango ya mazishi inafanyika huko nyumbani kwa mama yake na marehemu morogoro na taarifa rasmi zitatolewa baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Albert Mangwea mahali pema peponi. Amen

Jumanne, 28 Mei 2013

(News) Staki kusikia nyimbo zote za marehemu ALBERT MANGWEAR alizorekodi BONGO REC zikipigwa CLOUDS FM kuanzia sasa.

 Muda mfupi uliopita nilipokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anajulikana kwa jina la P Fuck Majani na kuniomba nipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.
Source Newz DJCHOKA

TRA imeteketeza shehena kubwa ya vipodozi vyenye viambata vya sumu.

<iframe width="420" height="315" src="http://www.youtube.com/embed/uD4efRE8O8U" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>

50 Cent ajitolea kugharamia mazishi ya mtoto wa kike wa miaka 14 aliyeuawa kwa risasi

Curtis Jackson a.k.a 50 Cent ameamua kufanya kitu kwaajili ya jamii kwa kujitolea kugharamikia mazishi ya mtoto wa kike mwenye miaka 14 aliyeuwawa kwa kupigwa risasi.

Weekend iliyopita rapper huyo alitoa pesa katika mfuko wake kwaajili ya familia ya mtoto huyo aitwaye D’aja Robinson aliyeuawa njiani akitokea katika party a sweet 16 huko Queens baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye basi.
Tukio hilo liliwagusa wengi akiwemo Curtis ambaye aliamua kwenda hadi kwa wazazi wa mtoto huyo na kujitolea kugharamia shughuli zote na kuhudhuria mazishi.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Curtis aliandika “Watu huwa wananipakazia picha mbaya kuhusu mimi, lakini mimi ni mtu wa kweli hapa duniani na sijasahau nilipotoka. Nimekuja kumsaidia huduma za mazishi ya huyu mtoto wa kike. Alikuwa mzuri, innocent na hakustahili kifo cha namna ile R.I.P D’Asia Robinson”
Kwa mujibu wa mtandao wa New York post, mtoto huyo alipigwa risasi kwa bahati mbaya sababu hakuwa mlengwa wa shambulio hilo.

WANAFUNZI WA SEKONDARI WAANIKA MATITI HADHARANI.....SOUTH AFRIKA CHEKI HAPA

Wazazi nchini afrika kusini walipigwa na butwaa baada ya kuwaona baadhi ya watoto wao wakionyesha matiti hadharani wakati wakishehrekea siku ya watoto nchini humo.

HIKI NDICHO KILICHOMUUA NGWEA

Habari kutoka kwa mtu wa karibu na Rapper Ngwea, aliejitambulisha kwa jina la Hamisi, amesema Ngwea alikua kule kwa mualiko wa kufanya show South Africa, ambapo alikua na msanii mwingine anaeitwa M to the P, na walitakiwa kuondoka leo kurudi Dar saa tatu asubuhi, lakini baada ya kuona hawatokei ndio wakaamua kwenda walipokuwa wamefikia na kuwakuta wote wawili wakiwa hawajielewi baada ya kujidunga madawa ya kulevya mengi (overdose), walipowahishwa hospitali, habari ndio ikawa hivi, kuwa Ngwea amefariki na M to the P yuko hoi hospitali
May God give you peace brother.

Feza Kessy aanza kung'ara katika jumba la Big Brother, apata bahati ya kuwa mkuu wa nyumba

Huwa wanasema nyota njema huonekana asubuhi, na asubuhi ya shindano la Big brother “The Chase” ilikuwa jana (May 27) ambapo nyota njema ya Feza ilionekana baada ya kupata cheo cha kuwa mkuu wa nyumba (Head Of House) katika Big Brother.

Jana (May 27) ikiwa ndio siku ya kwanza kati ya siku 91 za shindano hilo, ilikuwa ni mwanzo mzuri sana kwa mmoja wa wawakilishi wa Tanzania Feza Kessy baada ya kupata cheo hicho cha kuiongoza Diamond House.
Moja ya ukubwa wa cheo hicho cha Feza kama kiongozi wa nyumba ni uwezo wa kumuokoa mshiriki aliyekuwa nominated kutoka na kumweka mshiriki mwingine katika eviction.
Shindano la big brother linahitaji Technics nyingi kwa kila mshiriki ili aweze kuonekana na kusikika zaidi ya wenzake , kitu ambacho kinasaidia kuchukua attention ya watazamaji wengi ambao mwisho wa siku wao ndio hupiga kura .
Uchaguzi wa mkuu wa nyumba ya Diamond ulifanyika kwa washiriki wote kuchukua mpira mmoja ulioko katika box lililowekwa garden bila kuangalia na yeyote atakayechukuwa ‘winning ball’ ndio mshindi.

#BREAKINGNEWZ MSANI NGWEA AFARIKI DUNIA HUKO SOUTH AFRICA




NGWEA ENZI ZA UHAI WAKE  R .I .P

Jumatatu, 27 Mei 2013

CHRIS BROWN NA KARRUECHE TRANS WARUDIANA



Siku zote mwenye kiu iliyopitiliza akipewa maji ya kunywa hutamani atumie jagi zaidi ya kikombe anachowekewa maji, ndivyo ilivyomtokea mrembo Karrueche Tran aliyetoswa mwaka jana na Chris Brown aliyemchagua Rihanna dhidi yake wakati mrembo huyo akiwa na moyo uliojaa mapenzi na maumivu ya kulikosa penzi la ‘turn up the music singer’..
Sasa alipopewa nafasi tena ameamua kuitumia vyema na katika kupunguza zaidi umbali ameamua kuhamia kabisa nyumbani kwa mwimbaji huyo.

Kwa mujibu wa TMZ Chris na Karrueche wamekua wakiishi pamoja nyumbani kwa muimbaji huyo Los Angeles tangu walipoonekana pamoja kwenye sherehe ya kuzaliwa Chris Brown alipotimiza miaka 24.
Ripoti zinasema mrembo huyo amehamishia nguo zake na vitu vyake takribani vyote kutoka kwake na kuvipeleka nyumbani kwa Chris Brown lengo ni kuwa karibu zaidi na mwimbaji huyo.
Rafiki wa karibu wa KT ameuambia mtandao wa Hollywoodlife kuwa karrueche anajaribu kuweka commitment katika mahusiano yake na Chris ambayo mwimbaji huyo hawezi kuitunza lakini ameamua kujiweka kwenye mstari huo kwa ajili ya mahusiano yao.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa Karrueche anampenda Chris kwa sababu wanaendana na anapenda upande mwema wa Chris Brown.

Inawezekana Karrueche hamhofii tena Rihanna kwa kuwa mwaka jana alilazimika kuisomba mizigo yake kutoka kwenye nyumba ya mwimbaji huyo baada ya kumwagwa na himaya yake kuchukuliwa na RiRi bila sababu za msingi isipokuwa Chris kuamua tu kumrudisha RiRi.
Kwa sasa Chris na Rihanna hawako pamoja tena na Karrueche anaonekana kukaba nafasi yake vizuri. Swali, je hii pembe tatu ya mapenzi yaliyojaa drama itaishia hapo au baadae itambidi KT aondoe tena mizigo yake kumpisha Rihanna?



IRINGA:TAPELI ACHEZEA KICHAPO KIKALI TOKA KWA WANANCHI

Omba omba tapeli anayejifanya hana mikono akikamatwa na wananchi baada ya kukimbia
Wananchi eneo la Miyomboni wakiwa wamembana omba omba huyu tapeli kuonyesha mikono yake yote
” Huwa unasema wewe ni mlemavu huna mkono mmoja hii nini ….nyosha juu watu waone utapeli wako”
Hapa ni kipigo kikiendelea

Tapeli huyo akitaka kujinasua kutoka mikono ya wananchi wenye hasira kali
Hapa baada ya kupata upenyo akivaa nguo zake
Hapa akiwa ameachiwa na kuanza kutimua mbio

Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera 
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera 

AMA Kweli mwisho wa utapeli ni aibu kubwa na wahenga walinena kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo kwa wakazi wa Miyomboni mjini Iringa wamepata kushuhudia kituko cha mwaka baada ya watu waliochoka kuvumilia vitendo vya kitapeli vinavyofanywa mzee mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
Tapeli huyo mbali ya kuumbuliwa kwa kutakiwa kuonyesha miguu yake yote pamoja na mikono yake yote bado amepata kuchezea kichapo kiasi cha kunusurika kuuwawa na wananchi hao wenye hasira kali.
Tukio la mzee huyo kubainika kama ni tapeli kwa mara ya kwanza mtandao wa francisgodwin na matukiodaima ndio ulipata kufichua siri hiyo ya omba omba huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano wa mlemavu.
Kutokana na kufichuliwa kwa siri hiyo ya kujiigiza kuwa ni omba omba mlemavu wananchi wamekuwa wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na kumtimua mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua kumkimbiza kutoka eneo la Hazina Ndogo hadi miyomboni na kuanza kumpa kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo vyote kuwa si mlemavu.
Tapeli huyo mbali ya kujifanya ni mlemavu wa viungo wakati mwingine huwa anajifanya ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu mmoja na kuwaomba watu fedha za matibabu.
Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)
Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo kutokana na kichapo alichokipata na kuumizwa vibaya usoni.
Hata hivyo inasemekana mzee huyo amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali mbali kutokana na mbinu yake ya kufuru anayoifanya kuwa ni mlemavu wakati si mlemavu na kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya kiuchumi kuliko kuwaigiza walemavu na kuwa iwapo atarudia na kukutwa akifanya hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema wananchi hao ambao hata hivyo mtandao huu uliwaomba kufanya hivyo.
Aidha anadaiwa chanzo cha kichapo cha leo kwa mzee huyo tapeli ni mmoja kati ya mpenzi wake ambae alikuwa amemsusa na kuhamia kwa mpenzi mwingine kuueleza umma kuwa huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi wake ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea wananchi kufanya udadisi.
Kabla kufukuzwa na kuchezea kichapo tapeli huyo alifukuzwa eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya vijana wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada.